
Chama
cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa
Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia
uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni
kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa.
Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha,
inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria
zote.
“Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye
vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo
limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina
muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo.
Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru,
wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia
ni sawa na kuvunja sheria za nchi.
Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa chama chake kimefurahishwa
na barua hiyo kwa Waziri na kwamba nao pia wanafanya taratibu kumuona
ili kujadili mustakabali wa chama hicho.
Alisema kuwa TLS inaendelea na mchakato wa uchaguzi kama ulivyopangwa na
kuwataka wagombea wote kujiandaa kwa uchaguzi huo ambao alisema ni
halali.
Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika machi 18 mwaka huu, huku
wagombea kutoka vyama vya upinzani wakiwa wamejitokeza kuwania nafasi ya
uongozi wa juu
No comments:
Write comments