
Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni ameagiza kukamatwa kwa mwenyekiti Philipo
Komanya wa mtaa wa Kijitonyama baada ya kutuhumiwa kuhujumu mali za kata
wa mtaa wa huo .
Mwenyekiti
huyo alifungua akaunti mbili, ikiwa moja ya kwake nyingine ya serikali
ya mtaa na alikuwa anatumia zaidi ya kwake kwa mali za wananchi, Licha
ya kufungua akaunti hizo bado alikusanya 54,000 kwa ajiri ya mfereji
ambapo hakuweza kutekeleza kuukarabati mara baada ya kupata pesa hizo.
Katika
hatua nyingine kata hiyo imegundua maeneo 25 ya wazi ambayo yalikuwa
yanatumiwa na watu binafsi, baada ya kugundua hilo viongozi wa kata
wameweza kukusanya mapato shilingi milioni 57 katika maeneo 17 , huku
yakibakia maeneo 8 ambayo yanafanyiwa kazi ili kukusanya mapato hayo.
Hapi
ameagiza kuletwa kwa meneja katika soko la Mwenge ili kudhibiti mapato
ambayo yanapotea kwa wakusanyaji waliopo sasa. Pia ameagiza Manispaa
kupata shilingi 500 kwa kila kichwa kinachofanya kazi katika soko hilo .
Amewaomba wananchi kuacha tabia ya kuripoti matatizo yao kwa viongozi
wa juu badala yake wafuate utaratibu uliosahihi na satasaidiwa matatizo
yao.
No comments:
Write comments