Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako'
ameichambua ngoma wa msanii wa bongo fleva, Darassa inayokwenda kwa jina
la Muziki, na kusema kuwa msanii huyo ameimba vitu vya maana sana
kwenye ngoma hiyo.
Mchungaji Lusekelo ambaye amewahi kunukuliwa akitumia maneno ya wimbo
huo na nyingine kadhaa za bongo fleva katika mahubiri yake, alikumbana
na maswali katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, ambapo watu walitaka
kujua ni kwanini anatumia muziki wa kidunia katika mahubiri yake, badala
ya nyimbo za injili.
Akijibu maswali hayo, Mzee wa Upako amesema yeye kama mwanajamii,
anaishi duniani pamoja na wana jamii wengine, hivyo ni lazima ajue
matatizo yanayowazunguka watu wake ili aweze kuwasaidia na ndiyo maana
anajaribu kufuatilia mambo yanayopendwa na watanzanie ikiwemo muziki wa
kidunia.
"Muziki ni muziki, hakuna wa kanisani wala duaniani, cha msingi ni
ujumbe tu... Sasa ukisema wacha maneno weka muziki, kuna shida shida
gani? Ule muziki mi naupenda sana, anasema hakuna jambo gumu kama
kumfundisha chizi, na pia ni ujinga sana kusubiri embe chini ya mnazi.
Mimi nina nyimbo nyingi hata za kihindi nasikilizaga sana" Alisema
Mbali na ngoma ya Darassa, pia ametoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya
kuimba wimbo wa Navy Kenzo unaokwenda kwa jina la 'Kamatia Chini', huku
akishauri wasanii wa bongo fleva kuimba nyimbo zenye mafunzo badala ya
nyimbo za mapenzi pekee.
"Wasiimbe nyimbo za mapenzi tu, walipe pia sadaka kwa taifa... wakati mwingine waimbe na nyimbo ambazo zinaasa maadili"
Kuhusu Diamond na Alikiba, Mzee wa Upako amesita kusema ni yupi
anayemkubali zaidi, na kusema kuwa wote ni wa Mungu, na vipaji vyao
vimetoka kwa Mungu
No comments:
Write comments