Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro,
amesema miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu
za vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa
nyingi kwenye kazi yake.
Kamishna Sirro afichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha
East Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo,
anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.
Amesema kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani,
wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo
wakati mwingine humpigia usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za
uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.
"Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi". Amesema Kamanda Sirro
Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na
suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama
kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza na mara nyingi huwa
anachukua hatua.
No comments:
Write comments