Akizungumza
na mwandishi wetu baada ya kikao cha ngazi za juu za kanisa hilo
kilichofanyika juzi, Askofu mkuu wa kanisa hilo, Herryabwana Majebele
alisema amemsimamisha kazi mchungaji huyo kwa kuwa amechafua kanisa la
bwana.
Mchungaji
Msopela amekiri kufanya kosa hilo na amejitetea kwamba alipitiwa na
shetani, hivyo kuwataka waumini wamsamehe. Pia amemsihi Askofu Majebele
asimfukuze kanisani.
Hata
hivyo, Askofu Majebele alisema mchungaji huyo licha ya kulitumikia
kanisa kwa kipindi cha miaka sita, kitendo alichokifanya ni kuvunja Amri
10 za Mungu.
“Kumekuwa
na malalamiko mengi kutoka kwa waumini wakimtuhumu Msopela kuwabebesha
mimba wanawake wawili wa kanisa lake na kuwaahidi kuwaoa. Ushahidi upo
kutoka kwa waliotendewa vitendo hivyo, nimemfukuza kazi ya uchungaji ili
akaendelee na starehe zake huko kwingine,” alisema Majebele.
Baada
ya kumvua wadhifa huo, Askofu Majebele alisema kanisa hilo sasa
litakuwa chini ya uangalizi wa Mwinjilisti Malisafi Damasi hadi pale
atakapoletwa mchungaji mwingine.
Mmoja
wa waumini waliopewa mimba na mchungaji huyo, Sarah Muhayiwa alisema
alianza uhusiano wa kimapenzi naye tangu mwaka jana na kwamba baada ya
kubeba ujauzito, alianza kumshauri asiseme jambo hilo kanisani akiahidi
atamuoa.
“Baada
ya hapo alinipangishia chumba mjini Katoro tangu Januari 3 lakini
akanitelekeza, muda mfupi nikasikia ametangaza kumchumbia mwanamke
mwingine ambaye naye alikuwa na ujauzito wake,” alisema Sarah.
Mzee
wa kanisa hilo, Penina Thomas alisema mchungaji huyo amekuwa
akifumaniwa mara kwa mara na hivyo anapaswa kuondolewa kwenye nafasi
hiyo.
Mwinjilisti Damasi alisema kutokana na tabia hizo, waumini wengi wamekata tamaa ya kuendelea kuhudhuria ibada
Sunday, 26 February 2017
MAKUU YAMKUTA MCHUNGAJI ALIYEJAZA WAUMINI MIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments