Akizungumza leo katika mahojiano maalum na shirika la habari la Reuters,
Rais Trump amesema kuwa Marekani sasa hivi iko nyuma katika uwezo wake
wa silaha za atomiki.
Katika hatua nyingine, Reuters imemnukuu Trump akizungumza baada ya
mahojiano hayo, ambapo alieleza kuwa anachukizwa sana na kitendo cha
Korea Kaskazini kufanya majaribio ya silaha zake za maangamizi.
Alisema kuwa katika kuidhibiti Korea Kaskazini, Marekani inapaswa kutumia mfumo wa nchi marafiki kama Japani na Korea Kusini.
Ni nchi tisa pekee duniani zilizothibitisha kuwa na silaha za kinyuklia
ambazo ni Urusi, Marekani, China, India, Israel, Ufaransa, Korea
Kaskazini, Pakistan na Uingereza. Nchi nyingine zinazodaiwa kuwa na
silaha hizo zimekua zikikanusha vikali na kudai kuwa zinatumia nyuklia
kama nishati.
Kwa mujibu wa shirika linalojihusisha na masuala ya usalama,
Ploughshares Fund, linakadiria kuwa kuna zaidi ya silaha za nyuklia
15,000 duniani kote, ambapo Marekani na Urusi pekee zinamiliki zaidi ya
asilimia 93 ya silaha hizo
Friday, 24 February 2017
MAREKANI KUJENGA KINU KIKUBWA CHA SILAHA ZA NYUKLIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments