
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya
gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka
vibaya ambapo mmbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa
Mazingira luhaga mpina wilayani babati mkoa wa manyara.

Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa
babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia
katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mmbunge huyo na
kulazimika kumsubiri naibu waziri ambaye ameingia kumuona mbunge Gekul
na hapa naibu waziri Mpina anaeleza.
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira akalamika
kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa
babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua
umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari
kwaajili ya kubebbea taka lenye dhamani ya zaidi ya milioni 200.
No comments:
Write comments