
Kikosi maalumu cha kudhibiti dawa za kulevya wilaya ya Muleba mkoa wa
Kagera kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 14 wakiwemo watendaji na
wenyeviti wa serikali za vijiji wakilima dawa za kulevya aina ya
bangi,ukataji miti ya kupasua mbao, uchomaji mkaa,uwindaji haramu huku
wengine wakiojihusisha na uzalishaji wa pombe haramu aina ya gongo
kinyume cha sheria za nchi.
Operesheni ya kudhibiti dawa za kulevya,ujangiri,na uhalibifu wa
mazingira katika pori la akiba Burigi upande wa Muleba operesheni hiyo
imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na nyara za serikali akiwemo
mwenyekiti wa kitongoji cha nyantungu kata ya nyakabango bw.athuman
kanyamafa aliyekama twa akivuna mbao huku wawindaji haramu wakikamatwa
muda mchache baada ya kuuwa mnyama aina ya swala kinyume cha sheria za
nchi na walipohojiwa hali ilikuwa hivi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya
ya Muleba mhandisi richard ruyango ambaye anaongoza kikosi kazi cha
askari wa jeshi la wananchi,magereza,uhamiaji,polisi kwa kushirikiana na
wananchi amesema kuwa hata sita kuwachukulia hatua za kisheria
watendaji wa serikali wanaokiuka sheria,taratibu na kanuni za nchi.
No comments:
Write comments