Friday, 24 February 2017

UWOYA AFUNGUKA YA MOYONI MAHUSIANO YAKE NA NDIKUMANA

Kumekuwa na fununu za hapa na pale kuwa Irene Uwoya msanii mahiri wa filamu hapa nchini ameachana na mumewe Ndikumana huku akitajwa kutoka kimapenzi na wasanii kibao kama Diamond Platnumz, Msami, Dogo Janja na sasa Harmorapa.
Katika mahojiano na moja ya kituo cha runinga hapa nchini Uwoya amefunguka na kusema hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasanii wanaotajwa kwani kwa sasa hafikirii kuwa na mtu mwingine yoyote kwa kuwa bado anampenda mume wake Ndikumana na zaidi ya yote hawajaachana.

Akasema Mimi sijaachana na Ndikumana kwani sijawahi kupewa talaka ila nampenda sana mume wangu, saizi tuko mbali kwa sababu mimi niko busy na kazi na yeye yupo busy na kazi, kwa hiyo saizi nipo single sababu nampenda mume wangu”

No comments:
Write comments