Moto uliotokea katika kituo cha kulelea watoto
kinachosimamiwa na serikali, Guatemala umewaua takribani watoto kumi na
tisa huku wengine 25 wamejeruhiwa.Watoto takriban 60 wametoroka
wakisema kuwa wamekuwa wakinyanyasika.
''wakazi kadahaa wamesababisha moto huu katika maeneo mawili,
hivyo kikosi cha kuzima moto wakatumwa kupambana na moto huo na kusaidia
kutoa huduma ya kwanza,tumefanikiwa kuuzima kwa kutumia magaloni ya
maji zaidi ya 3000, kuna wakazi takriban 25 waliojeruhiwa''
Wabunge wa nchi hiyo wametaka uchunguzi wa haraka
kufanyika kuhusu tukio hilo katika kituo cha Guatemala .Huku rais wa
Guatemala,Jimmy Morales ametoa siku tatu za maombolezo.
Siku za
nyuma,makazi hayo yamewahi kupata lawama za kuwa kituo cha manyanyaso.
Makazi hayo yamekuwa yakitunza watoto wapatao takribani mia tano ambao
wamekuwa waathirika wa vurugu (ingawa eneo hilo lilitengenezwa kuwatunza
watoto mia nne pekee)
Wednesday, 8 March 2017
Watoto 20 wafa moto Guatemala katika kituo cha malezi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments