Tuesday 14 March 2017

UCL,LEICESTER CITY KUWAKARIBISHA SEVILLA KING POWER

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi za Pili
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto [2-0]
Leicester City v Sevilla [1-2]           
Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen [4-2]     
AS Monaco v Manchester City [3-5]     
++++++++++++++++++++++++++++
TAYARI Timu 4 zimeshatinga Robo Fainali ya UCL kufuatia kukamilika kwa Mechi zao za pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Wiki iliyopita na Wiki hii, Jumanne na Jumatano, zitapatikana Timy nyingine kutimiza idadi ya Timu 8.
Ijumaa hii Timu hizo 8 zitaingizwa kapuni kupanga Mechi 4 za Robo Fainali ambazo zitachezwa kuanzia Aprili 11.
Wiki iliyopita Timu 4 za kwanza kutinga Robo Fainali ni Mabingwa Watetezi Real Madrid, FC Barcelona, Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Kesho Jumanne zipo Mechi mbili ambapo Mabingwa wa Italy Juventus, walioshinda Mechi ya Kwanza 2-0 Ugenini, wapo kwao Juventus Stadium Jijini Turin, Italy kurudiana na FC Porto
Mechi nyingine Siku hiyo ni huko King Power Stadium wakati Mabingwa England Leicester City wakiwa kwao kujaribu kupindua kipigo cha 2-1 walichopewa na Sevilla ya Spain.
Jumatano zipo Mechi 2 pia ambapo Atletico Madrid wako kwao Vicente Calderon Jijini Madrid, Spain kulinda ushindi wa Ugenini wa 4-2 dhidi ya Wajerumani Bayer 04 Leverkusen.
Maechi nyingine ni huko France ambako AS Monaco wanapaswa kupindua kipigo cha 5-3 walichopewa na Manchester City.
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

No comments:
Write comments