Licha
ya watu wengi kuzungumza mengi kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam 'kuvamia' ofisi za Clouds Media kwa lengo la
kuwatisha vijana wachapakazi wanaopendwa mpaka na viongozi wa juu
serikalini, Shilawadu (Qwisa na Soud Brown), inaelezwa kwamba mkuu huyo
wa mkoa, hakwenda kwa shari.
Inaelezwa
kwamba alikwenda kufuatilia utaratibu wa documentary yake ya mwaka
mmoja madarakani, iliyofanyika pale Officers Mess, Oysterbay kwa sababu
anataka irushwe kwenye kituo hicho, ili watu wengi zaidi waone matunda
ya jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya na namna anavyoungwa
mkono na waathirika wenyewe.
Clip
inayosambaa, haioneshi popote kwamba mheshimiwa alitumia nguvu kuingia,
na zaidi kuna mtu anaonekana mapokezi ambaye ndiye aliyekuwa
akiwafungulia mlango wa ndani. Hakuna mtangazaji yeyote aliyepigwa na
kulikuwa na mazungumzo ya kawaida tu ambayo hata hiyo, haifahamiki
yaliishaje
Monday, 20 March 2017
Hiki ndicho alichokifuata Makonda clouds na si uvamizi kama inavyodaiwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments