Baada
ya kusikia maelezo ya Askofu Gwajima, na Ruge Mutahaba; yakithibitika
Ofisi ya Mwendesha mashtaka wa Serikali wanayo mashitaka ya wazi ambayo
yanaushahidi usio na shaka dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo
ni:
1.
Unyang'anyi wa kutumia silaha (armed robbery) kinyume na kifungu 287A
cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ya sheria zetu.
2.
Matumizi mabaya ya ofisi (abuse of office) kinyume na kifungu 96(1) cha
Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ya sheria zetu.
3.
Matumizi mabaya ya wadhifa (abuse of position) kinyume na kifugu cha 31
cha Sheria ya Kupambana na kuthibiti Rushwa ya mwaka 2007
4. Kuingia kijinai (Forcebly Entry) kinyume na kifungu 85 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu sura ya 16 ya sheria zetu.
5.
Kutishia kwa lengo la kulazimisha (intimidation) kinyume na kifugu 89B
cha Sheria ya Kanuni za Adhabu sura ya 16 ya Sheria zetu. shtaka la
kwanza halina kabisa dhamana.
Kama
ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka haikumuogopa marehemu Ukiwaona
Ditopile Mzuzuri (aliekua mkuu wa mkoa wa Tabora wakati huo, na mshenga
wa Rais Kikwete) na kumshitaki kwa mauaji, kitu gani leo kinawafanya
msimpeleke Mahakamani huyu Mkuu wa Mkoa wa Dar ambae wala sio mshenga wa
Rais?
âšjhnmallya2017
Monday, 20 March 2017
Baada ya maelezo ya Gwajima na Ruge, haya hapa makosa matano(5) mazito ambayo ndiyo kichinjio tosha cha kumchinja Makonda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments