Rais Magufuli: "Tumejielekeza
mno katika masuala ya udaku ambayo hayatuongezei chochote, hayatusaidii
chochote na ndio yanachukua muda wetu mwingi. Tuzungumze uchumi,
tujielekeze katika mambo ya maendeleo na hayana chama na nafurahi
kumuona mstahiki meya na ni wa CHADEMA.
Kampeni
zilishakwisha, ulie ugalegale Rais ni Magufuli. Ndio maana hii
interchange inajengwa kwenye jimbo la CHADEMA, nawaomba watanzania wa
vyama vyote tujifocus kwenye suala la maendeleo.
Mnahangaika
mnapost kwenye vipost vyenu, mpaka watu wengine wanaingilia uhuru
wangu, mimi huwa sipangiwi mambo. Mimi ni Rais ninayejiamini, siwezi
kupangiwa, hata siku ya kuchukua fomu nilienda mwenyewe.
Nitaamua
mwenyewe nani akae wapi, kwa hio Makonda wewe chapa kazi, nasema chapa
kazi. Najua wamenielewa, kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata
mimi naandikwa kwenye mitandao, Kwahio nijiuzulu Uraisi?
Mimi
ningefurahi hata kwenye mitandao tungekuwa tunapata ushauri jinsi ya
kufanya kazi, tunajadili personality na sio ideas, tuchape kazi kwa
manufaa ya watanzania.
Monday, 20 March 2017
MAGUFULI ATUPIA KAPUNI ISHU YA MAKONDA,......ATUMA DONGO ZITO KWA WANAOMPOST VIBAYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments