Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo
atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atakuwa
hafai kubaki kwenye nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu
yake katika nchi huru
Nape
ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo
kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,
cha kuvamia chombo cha habari cha Clouds, akiwa na askari wenye silaha
na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.
Waziri
huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye nchi
ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema
kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi.
"Tumezoea
kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwenda
kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili tunataka
kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini amefanya jambo
hili". Alisema Nape
Kufuatia
tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani
watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani
ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.
Pamoja
na hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT),
Dkt. Reginald Mengi amesema hawezi kutoa lawama kwa mtu yoyote mpaka
pale ukweli utakapofahamika japokuwa ameonekana kukerekwa.
"Kwetu sisi hili ni jambo ni la hatari sana, linatuogopesha na linatishia maisha ya waandishi wa habari". Alisema Dkt. Mengi
Kwa
upande mwingine Mengi amewasihi waandishi wa habari kutokuwa waoga kwa
jambo lolote wanalopambana nalo ila wanachopaswa ni kufanya kazi kwa
kufuata misingi iliyowekwa
Monday, 20 March 2017
licha ya Magufuli kumkingia kifua Makonda,........Nape naye avimba kiume, haya ndiyo aliyoamua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments