Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu jana alishikiliwa na jeshi
la polisi kwa saa kadhaa wilayani humo akihusishwa na vurugu zilizoibuka
ndani ya kikao cha ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dk. Nagu ambaye alikuwa mmoja kati ya wajumbe wa kikao cha kamati ya
siasa ya wilaya ya Hanang, alishikiliwa na jeshi la polisi baada ya
kutokea mvutano mkali wa pande mbili zilizoibuka wakati wa mjadala wa
kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa ndani wa chama
hicho.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Francis Masawe alithibitisha
kukamatwa kwa Dk Nagu kutokana na vurugu hizo na kueleza kuwa aliandika
maelezo na kuachiwa baada ya saa kadhaa.
“Taarifa ambazo nimezipata ameachiwa baada ya kuandika maelezo na
tayari walifikia makubaliano wenyewe [pande mbili zilizosigana],”
Kamanda Masawe anakaririwa na Mwananchi.
Dk. Nagu aliwahi kuwa waziri wa viwanda na biashara, pamoja na waziri
wa katiba na sheria kwa nyakati tofauti katika awamu mbili za serikali
zilizopita
Tuesday, 18 July 2017
DK MARY NAGU AONJA JOTO YA JIWE AKAMATWA NA POLISI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments