Tuesday, 18 July 2017

Waziri: Asilimia 90 ya watoto hufundishwa ‘ushoga’ shuleni



Waziri wa maadili wa Uganda, Simon Lokodo amesema kuwa asilimia 90 ya watoto nchini humo hufunzwa kwa siri jinsi ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, akikemea kitendo hicho.
Waziri Lokodo ambaye anafahamika zaidi kwa msimamo wake juu ya vitendo vilivyo kinyume na maadili ikiwa ni pamoja na uvaaji usiofaa, amenukuliwa wakati Bunge la Uganda lilipokuwa likijadili usalama wa watoto.

Ingawa hakukuwa na taarifa ya kina kuhusu tamko la waziri huyo, kauli yake imenukuliwa na akaunti rasmi ya twitter ya Bunge la nchi hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi. Lukodo alilitaja jiji la Kampala kama jiji ambalo linaongoza kwa mmomonyoko wa maadili nchini humo.

Uganda ni moja kati ya nchi ambazo zimeweka sheria kali dhidi ya tabia za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na uvaaji wa sketi fupi kwa wasichana na wanawake.

Katika hatua nyingine, Bunge hilo liliidhinisha kuanzishwa kwa Kamati Maalum ya kupambana na picha na video za ngono (pornography), Kamati itakayokuwa chini ya wizara ya maadili.

No comments:
Write comments