Wednesday, 19 July 2017

KWISHAA!!!! SIMBA YAFUNGA KAZI YAMALIZA UKUTA WOTE WA STARS



Image result for SAID MOHAMED NDUDA NA ERASTO NYONI 
Simba imemsajili beki wa kiraka, Erasto Nyoni kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyoni amejiunga na Simba akitokea Azam FC ikiwa ni siku chache baada ya kufanya vizuri katika michuano ya Cosafa.

Kitu kizuri kwa Nyoni ni uwezo wake wa kucheza namba zote nne za ulinzi.

Pia anaweza kucheza nafasi ya kiungo mkabaji kwa ufasaha hali inayomfanya kuwa na nafasi kubwa ya kucheza.

Nyoni alirejea nchini na kujiunga na Azam FC akitokea Vital'O ya Burundi
PIA

Simba imemsajili kipa Said Mohammed kutoka Mtibwa Sugar.


Said maarufu kama Nduda, amesajili Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Katika michuano ya Cosafa iliyoisha hivi karibuni na Taifa Stars kushika nafasi ya tatu, Nduda aliibuka kipa bora wa michuano hiyo ingawa alidaka mchezo mmoja tu wa kuwania mshindi wa tatu

No comments:
Write comments