Kiungo wa pembeni wa Azam FC, Ramadhani Singano amefuzu vipimo vya afya vya klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco.
Difaa
Al Jadida ilimtumia mwakilishi wake nchini kumfanyia Singano maarufu
kama Messi vipimo vya afya na taarifa zimeeleza kuwa amefuzu.
"Sasa
ni suala la viza tu, kama hili likikamilika, basi Singano ataondoka.
Hawataingia naye mkataba sasa hivi hadi mkataba wake na Azam FC
utakapoisha siku chache zijazo.
"Ila kuna taarifa nimeambiwa wamemtaka kwenda kule mapema ili kuzoea mazingira," kilieleza chanzo.
Mkataba
wa Singano na Azam FC umebakiza siku chache kwisha na hivi karibuni
ilielezwa mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya Azam FC
BOFYA HAPA KUONA KWA KINA UNDANI WA HABARI HIIMCHEZAJI MPYA WA YANGA ATOBOA SIRI NZITO
BOFYA HAPA KUONA KWA KINA UNDANI WA HABARI HIIMCHEZAJI MPYA WA YANGA ATOBOA SIRI NZITO
No comments:
Write comments