Mshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahim Ajibu, hataipata jezi aliyokuwa anaitumia Simba.
Tayari ameshauriwa kutafuta namba nyingi na si 23 ambayo inatumiwa na lejendari wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Ajibu
amesaini Yanga miaka miwili na usajili wake umezuia gumzo huku ukiamsha
morali ya Wanayanga ambao walionekana kukata tamaa wakati Simba
ikisajili mfululizo.
Jezi namba 23 upande wa Yanga tayari inaonekana ina mwenyewe. Cannavaro anajulikana kama “Baba Mwenye Nyumba”.
Hii inatokana na kuwa Yanga kwa muda mrefu pia ni kati ya manahodha wa muda mrefu.
No comments:
Write comments