Sunday, 5 March 2017

MAMA AKE WEMA SEPETU AKAMATWA NA POLISI


Mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariam jana alikamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam akituhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyiffu kutoka kwa mfanyabiashara, Alex Msama.

Kwa mijibu wa gazeti la Mwananchi, Mariam alikamatwa majira ya saa nne asubuhi na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay jana ambapo alifunguliwa jalada la kesi inayomkabili. 
Baadaye aliachiwa kwa dhamana saa 12 jioni baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.

Inadaiwa kuwa chanzo ni kuwa, Mariam alikubali kumuuzia Msama nyumba iliyopo Sinza, Dar es Salaam baada ya benki ya TIB kutaka kuipiga mnanda kufuatia mama Wema Sepetu kumdhamini mtu katika benki hiyo ambaye hakurejesha mkopo wake.

Kwa sababu Msama hakuwa na fedha ya kutosha kwa wakati huo, aliendelea kutafuta fedha katika benki na wakati huohuo akimpa Mariam fedha kidogo ambazo zilifikia TZS milioni 14. 
Mariam baada ya kuona mchakato wa Msama unachelewa, aliuza nyumba ile kwa mtu mwingine bila kumtaarifa Msama aliyekuwa tayari amechukua fedha zake.

Aidha, jana wakati wa mahojiano Kituo cha Polisi, Mariam alikiri kupewa TZS milioni 8 ambazo zipo kimaandishi na kusema hatambui fedha nyingine zaidi.

Msama alipoulizwa kuhusu kumshtaki Mariam alikiri na kusema kuwa yeye anataka kulipwa fedha zake zote.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu alithibitisha kushtakiwa kwa kada huyo na kusema aliandika maelezo ya awali kuhusu suala hilo na kuachiwa.

No comments:
Write comments