Aliwataka waumini wasichanganywe na maneno kwani taratibu na katiba ilifuatwa katika kumuondoa Mokiwa.
"Nawaomba waumini wa kanisa hili kuwa watulivu, msichanganye na maneno
yanayosemwa juu ya uamuzi wa kumtaka Dk Mokiwa kujiuzulu.Tulifuata
taratibu zote na hivi sasa mimi ndiye msimamizi mkuu wa dayosisi hadi
hapo askofu wa jimbo atakapopatikana," amesema Dk Chimeledya
Dk Chimeledya ametoa msisitizo huo leo wakati aliposhiriki ibada ya misa
ya asubuhi iliyoongozwa na Jaji mstaafu Augustino Ramadhan
iliyofanyika katika kanisa la St Albano Posta na kusema kuwa Katiba
inaruhusu yeye kulisimamia kanisa kutokana na Mokiwa, kutakiwa kujiuzulu
.
Amesema mchakato wa kumuamuru Dk Mokiwa aliyekuwa askofu mkuu wa
dayosisi hiyo ulifuata sheria , kanuni na katiba ya Anglikana
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004
Sunday, 26 February 2017
ASKOFU CHIMELEDYA;WAUMINI MSICHANGANYWE NA MANENO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments