Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa watoto hao watatu wanaendelea vizuri na kwamba kwa sasa wako katika hatua za mwisho za ufanyaji mazoezi ya viungo.
“Watoto hawa wanatarajia kuwasili ijumaa katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro Internatinal Airport (KIA) hivyo, nawaomba wananchi na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi tukawapokee watoto wetu na kuwafariji, kiafya wanaendelea vizuri kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kufanya mazoezi,” amesema Nyalandu. Aidha, kuhusu ufadhili walioupata wa kusomeshwa na wafadhili mpaka chuo kikuu, amesema kuwa hayo yatakuwa ni makubaliano kati ya wazazi wao na wafadhiri ambao wataamua kama waendelee kusoma hapa hapa nchini au Marekani
No comments:
Write comments