Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.
1.
Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la
mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni
wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya
zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).
Niliambiwa
walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa
wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya
kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).
Niliambiwa
wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba
ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka
hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho
kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.
2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k
3.
Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na
kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa
ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.
4.
Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza
kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza
kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani.
Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa
katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki.
Ndio
maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki
wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama
Jesuits.
Jesuit
Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu
zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa
katoliki.
5.
Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu
na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na
mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila
Lucifer aonekane mbaya.
6.
Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna
daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika
imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu
kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)
7. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi.
Wafuasi
wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini
manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini
wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge
zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu
wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.
8.
Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri,
yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya
utawala
Friday, 24 March 2017
HISTORIA FUPI YA FREEMASON
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments