Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amemfungulia mashitaka
matano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo ameyawasilisha
kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Makonda ni pamoja na kughushi vyeti,
kupokea zawadi bila kutangaza, jambo ambalo ni kinyume na sheria za
utumishi wa umma, kujipatia mali kutoka kwa watuhumiwa wa biashara ya
madawa ya kulevya, kuwadhalilisha watu kwa kuwataja kwenye tuhuma za
madawa ya kulevya bila kuwa na vielelezo na kutumia madaraka vibaya.
Hatua hiyo ya meya Jacob, imekuja siku chache baada ya mkuu huyo wa
mkoa, kudaiwa kuvamia kwenye ofisi za Clouds Media, kushinikiza kipindi
kilichorekodiwa kikiwa na habari ya Mchungaji Josephat Gwajima, kirushwe
hewani wakati kipindi cha Shilawadu kikiendelea.
Kitendo hicho kilimlazimu Waziri Nape Nnauye, mwenye dhamana ya
kuwalinda waandishi wa habari, aunde tume maalum kuchunguza sakata hilo,
ambayo ilipewa muda wa saa 24 kukamilisha kazi yake, lakini mpaka sasa
bado ripoti yake haijatok
No comments:
Write comments