Kegera Sugar hawaelewi lolote kuhusiana na mshambuliaji Mbaraka Yusuf, wanasema ni mali yao.
ikumbukwe simba walisema mchezaji huyo ni wao na walimpeleka kagera kwa mkopo na kagere wakasema walimalizana na simba kuhusu mchezaji huyo
Msisitizo wa Kegera Sugar wanasema wanataka walipwe shilingi milioni 150
ili imuachie mshambuliaji huyo kwenda Azam FC ambako tayari amesaini.
Hatua hiyo imekuja siku chache tangu Meneja wa Kagera, Mohammed Hussein
kupiga hodi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akidai
mshambuliaji huyo amesajiliwa kimakosa.
Mbaraka alisaini mkataba wa kuichezea Azam hivi karibuni kwa dau la
zaidi ya shilingi milioni 40 akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka ndani ya
uongozi wa Kagera, mshambuliaji huyo aliingia makubaliano ya kusaini
mkataba wa miaka miwili akiwa bado amebakiza mwaka mmoja.
Mtoa taarifa huyo alisema uongozi wa Kagera umekubali kumuachia
mshambuliaji huyo kwa makubaliano ya kulipwa shilingi milioni 150 ambazo
wanazihitaji wao.
Aliongeza kuwa, kama Azam hawatakubali kutoa fedha hizo, basi suala hilo
litafika mbali ikiwemo Fifa kutokana na timu hiyo kumsainisha mchezaji
akiwa ana mkataba bado wa miaka miwili.
Alipotafutwa Meneja wa Kagera, Mohammed Hussein kuzungumzia hilo, alikiri mchezaji huyo kuwa na mkataba na Kagera na kusema wameshapeleka malalamiko yao kwa TFF juu ya kitendo hicho
No comments:
Write comments