Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Monday, 9 October 2017

WAKILI WA LEMA ARUDI NYUMA KATIKA KESI INAYOMKABILI MBUNGE HUYO AKIDAIWA KUMKASHIFU RAIS


Wakili Sheck Mfinanga amejitoa kumwakilisha mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katika kesi ya uchochezi akidaiwa kumkashifu Rais John Magufuli akisema haridhishwi na mwenendo wa shauri hilo.

Mfinanga amejitoa ikiwa ni siku chache baada ya hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo kujitoa kutokana na kuwekewa pingamizi na upande wa Jamhuri kuwa ana urafiki na Neema ambaye ni mke wa Lema.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Desdery Kamugisha, wakili huyo amesema moja ya sababu ni kutokana na upande wa utetezi kutopewa jalada la mwenendo wa kesi licha ya kuwasilisha maombi mara tatu mahakamani hapo.

“Kwa kuwa nimeshaleta notisi ya kukata rufaa naomba iingie kwenye rekodi, najitoa kuendelea kumwakilisha mteja wangu kutokana na kile ninachokiona kisheria kwamba tumeomba proceedings (mwenendo wa kesi) na imeshindikana. Mimi si wakili wake tena, nimejitoa,” amesema.

Baada ya ombi hilo, Mfinanga alikusanya nyaraka zake, alimuaga mteja wake na kunyanyuka kwenye kiti alichokuwa ameketi na kutoka ndani ya chumba cha Mahakama.

Hakimu Kamugisha alimpa nafasi Lema ya kuzungumza naye alisema amemsikiliza wakili wake na hana pingamizi juu ya ombi hilo.

Hata hivyo, amesema kwa ufahamu wake ni kwamba, hii ni mara ya tatu upande wa utetezi umeomba jalada la mwenendo wa kesi lakini hawajapewa na kwa sababu hiyo hana imani na hakimu.

“Mheshimiwa nilishasema sina imani na wewe kama mtu niliyekuwa nimemwajiri kunisaidia katika masuala ya kisheria anaweza kutilia shaka na nilisema hadharani, basi naomba nipewe muda wa kutafuta wakili mwingine,” amesema.

Lema amesema anaomba kupatiwa nyaraka zote za kesi na muda wa kutafuta wakili mwingine.

Baada ya ombi hilo, Wakili wa Serikali, Khalili Nuda alisema ni haki ya kikatiba ya mshtakiwa kuwakilishwa mahakamani. Aliiomba mahakama impatie muda wa kutafuta wakili mwingine.

Nuda ameiomba Mahakama impatie mshtakiwa muda muafaka wa kutafuta wakili mwingine.

Hakimu Kamugisha amesema wakili wa mshtakiwa amejitoa wakati kesi ilipotajwa kwa ajili ya kusikilizwa, hivyo Lema anapewa muda wa kutafuta mwingine. Aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 14.

Mwananchi:

Thursday, 5 October 2017

BAADA YA KIMYA KIREFU SASA FAMILIA YA TUNDU LISSU YATOA TAMKO YATAKA WAPELELEZI WA KIMATAIFA




Ndugu zake Tundu Lissu, Vincent Mughwai(kushoto) na Alute Mughwa (kulia)
Image captionNdugu zake Tundu Lissu, Vincent Mughwai(kushoto) na Alute Mughwa (kulia)

Familia ya mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, imeiomba serikali kuongeza kasi ya upelelezi wa kesi ya kushambuliwa kwa mbunge huyo wa Singida mashariki aliyepigwa risasi mnamo mwanzoni mwa mwezi jana huko mjini Dodoma.
Familia hiyo iliyowakilishwa na kaka zake wawili, wameitaka serikali kuvishirikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa kama vinavyoshirikishwa katika mambo mengine ili kuongeza ufanisi katika upelelezi huo.Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya thelathini na watu ambao mpaka sasa hawafahamiki pindi alipokuwa mjini Dodoma akihudhuria vikao vya bunge.
Kwa upande wake, katika siku za hivi karibuni, jeshi la polisi nchini Tanzania lilisema upelelezi wa tukio hilo unasuasua kutokana na dereva wa Mbunge huyo kutofika polisi kutoa ushahidi.Hata hivyo, taarifa kutoka Chadema zinasema kuwa dereva wa mbunge huyo yuko nchini Kenya kwa ajili ya kupata matibabu ya kisaikolojia kutokana msongo wa mawazo alioupata baada ya kisa hicho.

Kufuatia kauli hiyo, familia hiyo imeliomba jeshi la polisi kufanya utaratibu wa kumfuata dereva huyo mjini Nairobi kwa ajili ya mahojiano ili uchunguzi uendelee.
Tundu Lissu yuko nchini Kenya kwa takribani wiki nne sasa ambako anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi aliyoyapata kutokana na shambulio hilo.

Sunday, 30 July 2017

CHADEMA YAFUNGUKA ISHU YA MWANDISHII WA TBC KUZUIWA KUCHUKUA HABARI KATIKA MAKAO MAKUU YA CHADEMA

Image result for JOHN MREMA
Kuhusu Mwandishi wa TBC kuzongwa /kuzuiliwa kutimiza wajibu wake.
Tumepokea kupitia vyombo vya Habari taarifa za tukio la Mwandishi wa habari wa TBC kushindwa kutimiza wajibu wake Katika Makao Makuu ya CHADEMA.

Tunapenda kuweka wazi Kuwa tukio hili halikufanywa kwa maelekezo ya kiongozi yeyote na kama Chama hatujawahi na hatuna Sera wala msimamo wa kubagua chombo chochote cha habari.

Kwa hatua za awali tunafanyia uchunguzi tukio hilo ili kuweza kubainisha Nini hasa kilitokea Katika siku hiyo na tunategemea kupata ushirikiano kutoka kwa Mwandishi husika Katika uchunguzi wetu.

Tunapenda kuwahakikishia waandishi wote wa habari kuwa wataendelea kuwa salama Katika matukio yote ambayo yatakuwa yakifanywa na CHADEMA na watapata ushirikiano unaostahili.

Baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutatoa taarifa Kamili juu ya tutakachokuwa tumebaini na hatua tutakazochukua .
Sisi tunaamini Katika uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa waandishi wa habari na haki ya kupata na kutoa habari/taarifa kuwa ni nguzo kuu katika kujenga taifa la kidemokrasia na hatimaye kufikia maendeleo ya kweli.

Imani yetu hiyo tumekuwa tukiidhihirisha kwa vitendo hadharani, mfano, CHADEMA ni taasisi ya kwanza ya kisiasa iliyotia saini na kukubaliana na *Azimio la Dar es Salaam Juu ya Uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji* (hatuna uhakika kama ipo nyingine iliyofanya hivyo hadi sasa).

Tunapenda kutumia fursa hii kuwahakikishia wadau wote wa habari, wakiwemo waandishi, wahariri na wananchi, kuwa tutaendelea kuionesha imani hiyo kwa vitendo katika shughuli zetu zote za kisiasa.

Pamoja na salamu za Chama.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA

Thursday, 20 July 2017

Video: Watoto 3 walionusurika ajali ya Lucky Vicent kurejea nchini


Watoto watatu walionusurika katika ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya msingi Lucky Vicent wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi wa 8, 2017 wakitokea Marekani walikopelekwa kwa ajili ya matibabu mara baada ya ajali hiyo.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa watoto hao watatu wanaendelea vizuri na kwamba kwa sasa wako katika hatua za mwisho za ufanyaji mazoezi ya viungo.



“Watoto hawa wanatarajia kuwasili ijumaa katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro Internatinal Airport (KIA) hivyo, nawaomba wananchi na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi tukawapokee watoto wetu na kuwafariji, kiafya wanaendelea vizuri kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kufanya mazoezi,” amesema Nyalandu. Aidha, kuhusu ufadhili walioupata wa kusomeshwa na wafadhili mpaka chuo kikuu, amesema kuwa hayo yatakuwa ni makubaliano kati ya wazazi wao na wafadhiri ambao wataamua kama waendelee kusoma hapa hapa nchini au Marekani

TUNDU LISU AKAMATWA AIRPORT

Moja ya Habari zilizotufikia kutoka Dar es Salaam ni kuhusu Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika ‘TLS’ ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu kukamatwa na Polisi akiwa Airport Dar es Salaam akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.

Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.

Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema,  John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa  jioni hii.

Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Wednesday, 19 July 2017

ZITTO ATAKI MASIHARA KWENYE MASUALA YA KITAIFA.............ACHAFUKWA AMTOLEA UVIVU TUNDU LISSU,


SeeBait
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amekuja juu na kutoa ya moyoni akionekana kutofurahishwa na taarifa iliyosambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandaoni ikitokea Chama cha demokrasia na maendeleo- CHADEMA.

Kauli za Zitto zilifuatia taarifa aliyoiona kwenye ukurasa wa Twitter  iliyosema; “CHADEMA waitaka Jumuiya ya kimataifa kuinyima misaada Tanzania kutokana na ukiukwaji wa Demokrasia mfano, kukamatwa kwa viongozi wa upinzani”

Baada ya kuiona hiyo taarifa Zitto Kabwe aliandika “Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia .NDANI”

Baada ya Zitto kuonyesha dhahiri msimamo wake, baadhi ya Followers wake kwenye Twitter walimuandikia kila mmoja na maoni yake na yeye akawajibu kama inavyoonekana hapa chini.