Kuhusu Mwandishi wa TBC kuzongwa /kuzuiliwa kutimiza wajibu wake.
Tumepokea kupitia vyombo vya Habari taarifa za tukio la Mwandishi wa
habari wa TBC kushindwa kutimiza wajibu wake Katika Makao Makuu ya
CHADEMA.
Tunapenda kuweka wazi Kuwa tukio hili halikufanywa kwa maelekezo ya
kiongozi yeyote na kama Chama hatujawahi na hatuna Sera wala msimamo wa
kubagua chombo chochote cha habari.
Kwa hatua za awali tunafanyia uchunguzi tukio hilo ili kuweza kubainisha
Nini hasa kilitokea Katika siku hiyo na tunategemea kupata ushirikiano
kutoka kwa Mwandishi husika Katika uchunguzi wetu.
Tunapenda kuwahakikishia waandishi wote wa habari kuwa wataendelea kuwa
salama Katika matukio yote ambayo yatakuwa yakifanywa na CHADEMA na
watapata ushirikiano unaostahili.
Baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutatoa taarifa Kamili juu ya tutakachokuwa tumebaini na hatua tutakazochukua .
Sisi tunaamini Katika uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa waandishi wa
habari na haki ya kupata na kutoa habari/taarifa kuwa ni nguzo kuu
katika kujenga taifa la kidemokrasia na hatimaye kufikia maendeleo ya
kweli.
Imani yetu hiyo tumekuwa tukiidhihirisha kwa vitendo hadharani, mfano,
CHADEMA ni taasisi ya kwanza ya kisiasa iliyotia saini na kukubaliana na
*Azimio la Dar es Salaam Juu ya Uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji*
(hatuna uhakika kama ipo nyingine iliyofanya hivyo hadi sasa).
Tunapenda kutumia fursa hii kuwahakikishia wadau wote wa habari,
wakiwemo waandishi, wahariri na wananchi, kuwa tutaendelea kuionesha
imani hiyo kwa vitendo katika shughuli zetu zote za kisiasa.
Pamoja na salamu za Chama.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA
Sunday, 30 July 2017
CHADEMA YAFUNGUKA ISHU YA MWANDISHII WA TBC KUZUIWA KUCHUKUA HABARI KATIKA MAKAO MAKUU YA CHADEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments