Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imethibitisha
ripoti kuwa raia kadha wa Nigeria wamefukuzwa kutoka nchini humo.
Vyombo vya habari nchini Nigeria vimekuwa vikiripoti kuwa raia 97 wa
Nigeria wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu tofauti walifukuzwa kutoka
Afrika Kusini siku ya Jumatatu.
asema
kuwa mamia ya watu wasio na vibali walisafirishwa kutoka nchini humo,
wengi wao kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC.
Wengine ni raia wa Pakistan, China, Bangladesh na Somalia.
Afrika Kusini imekumbwa na ghasia dhidi ya raia wa kigeni na visa vya kuporwa kwa maduka yanayomilikiwa na wahamiaji.
Afrika Kusini huwafukuza karibu watu 30,000 kila mwaka
No comments:
Write comments