Kwa msanii au mtu maarufu, kinga pekee inayomsaidia kuendelea kuwa na
heshima yake, ni kuwa na wimbo unaofanya vizuri ama kuwa na fedha.
Anapokosa hivyo, mambo hubadilika na hapo ndipo ule usemi wa Fid Q kuwa
usupastaa ni mzigo wa miiba huwa na maana. Hussein Machozi anaijua hali
hiyo na kupitia mitihani aliyopitia miaka miwili iliyopita, amejifunza
mengi.
“Nimejifunza kuna watu wa kweli na kuna watu feki,” Machozi amesema.
“Kuna watu wa kweli ambao wamekaa na mimi kwa shida mpaka sasa hivi wapo
na mimi, marafiki wa kweli. Na kuna watu baadhi ambao walikuwa wapo
karibu sana na mimi kipindi nipo juu, lakini kipindi ambacho nilikuwa
kimya kwa muda mrefu, wameniacha mbali wamenitupa,” anasema.
“Wamenisahau,wameninyanyasa, imefikia kipindi wengine wanatongoza mpaka
mke wangu. Ni kitu ambacho kinauma sana na sio kwamba mtu anamtongoza
mtu hamjui, anamtongoza anajua kabisa huyu ndio future ya Hussein
Machozi, yaani ndio mtu anayemtegemea. Siwasemi wengine ni mabosi
walikuwa wanajifanya mabosi na vitu kama hivyo. Lakini yote tupilia
mbali, ni kwamba mimi nasonga mbele na maisha naendelea na maisha yangu,
nimesahau mabaya yote, nimefungua ukurasa mpya.”
No comments:
Write comments