Monday 27 March 2017

Dadake Fidel Castro afariki dunia


Dadake mdogo wa aliyekuwa kiongozi wa Cuba, Fidel Castro, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Agustina Castro Ruz hakushiriki katika siasa chini ya ndugu zake wawili, Fidel na Raul ambaye alimrithi Fidel kama rais wa taifa hilo.

Aliolewa na mpigaji kinanda Silvio Rodriguez, aliyelalamika kuhusu uhusiano mgumu na familia ya mkewe.

Rodriguez alihamia Marekani miaka ya 1990, Fidel Castro alifariki dunia mwaka jana.
Dadake mkubwa wa Fidel, Angela Castro alifariki dunia mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 88.

No comments:
Write comments