Saturday 11 March 2017

EPL YAENDELEA WIKIEND HII VIGOGO WAPO FA CUP

WIKIENDI hii Mashabiki wa Soka la England watashuhudia Mechi mchanganyiko za EPL, Ligi Kuu England, na zile za EMIRATES FA CUP ambayo ipo Robo Fainali.
Jumamosi zipo Mechi 3 za EPL na 2 za FA CUP.
Kwenye Ligi, Bournemouth, ambao Wiki iliyopita waliibana Man United na kupata Sare 1-1 huko Old Trafford lakini Beki wao Tyrone Mings akafungiwa Mechi 5, wapo Nyumabani kuivaa West Ham.
Mechi nyingine za Ligi ni Everton na West Brom na ile ya Hull City na Swansea City.
Kwenye FA CUP hiyo Jumamosi ni Middlesbrough na Man City huko Riverside wakati Arsenal ikiwa kwao Emirates Jijini London kucheza na Timu isiyokuwa kwenye Mfumo rasmi wa Ligi Lincoln City.
Jumapili EPL ina Mechi tu huko Anfield kati ya Liverpool na Burnley na FA CUP itachezwa huko White Hart Lane kati ya Tottenham na Millwall.
Jumatatu Usiku Mechi pekee ni mtange mkali wa FA CUP huko Stamford Bridge kati ya Wenyeji Chelsea na Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Man United.
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumamosi Machi 11
1800 Bournemouth v West Ham United           
1800 Everton v West Bromwich Albion            
1800 Hull City v Swansea City     
Jumapili Machi 12
1900 Liverpool v Burnley            
FA CUP
Ratiba
Raundi ya 6 [Robo Fainali]
**Saa za Bongo
Jumamosi Machi 11
1515 Middlesbrough v Man City
2030 Arsenal v Lincoln City
Jumapili Machi 12
1700 Tottenham Hotspur v Millwall
Jumatatu Machi 13
2245 Chelsea v Manchester United

No comments:
Write comments