Mambo yanayomtokea kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ni kama mchezo wa kuigiza.
Jana,
Lissu alianza siku kwa furaha baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa
Kisutu kumuona hana kesi ya kujibu, lakini dakika chache baadaye polisi
walimkamata tena, kumhoji na kumuachia kwa dhamana.
Licha
ya kashikashi hizo mahakamani na kituo cha polisi, Lissu ameonyesha
kuwa na sakata jingine katika uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa
Tanganyika (TLS) baada ya kudai kuwa kuna mkakati unasukwa na baadhi ya
mawakili wenzake kutaka kumkwamisha asigombee urais wa chama hicho.
Baada
ya kuachiwa huru, Lissu alikamatwa na polisi akiwa Mahakama ya Kisutu
na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi, lakini haikueleweka sababu za
kukamatwa kwake.
Lissu alikutana na
polisi hao saa 4:00 asubuhi na akaambiwa kuwa anahitajika kituoni,
mbunge huyo aliomba aendeshe gari lake mwenyewe ambalo alikuwa nalo
Kisutu.
Wakili wake, Fredrick Kihwelo
alisema: “Polisi walikubaliana naye na kuingia kwenye gari lake na
kuelekea kituoni hapo na walipofika walikaa muda kisha wakaelezwa kuwa,
anadaiwa kutoa
matamshi yanayoweza kusababisha matatizo ya kidini.”
Alisema
Lissu alidaiwa kutoa matamshi hayo akiwa mkoani Dodoma, hivyo baada ya
mahojiano aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo Machi
13
matamshi yanayoweza kusababisha matatizo ya kidini.”
No comments:
Write comments