Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima Joseph Gwajima
“Isingekuwa busara watu wavamiwe na mimi ni mhusika mkuu halafu nisije kutoa pole,” alisema
Hatua ya Gwajima imekuja baada ya tukio la kituo hicho kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa na polisi wenye silaha.
Gwajima amewasilia saa 4:00 asubuhi akiwa na msafara wa magari zaidi ya manne na walinzi wake takribani 30 na alipofika alipokelewa na Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na kufanya mazungumzo na waandishi wa habari na baadaye na uongozi wa kituo hicho.
Amewataka Clouds kuendelea na kazi zao za kawaida na kutaka suala hilo lisichukuliwe kisiasa huku akikisitiza kuwa Mkuu wa mkoa alikosea
No comments:
Write comments