Wednesday, 22 March 2017

"Makonda aliwatishia watangazaji wa Clouds kuwafunga miezi 6 au kuwataja kwenye dawa za kulevya"- Kamati


Ripoti ya kamati hiyo imesomwa mbele yaWaandishi wa habari na Mwakalikishi wa kamati hiyo Deodatus Balile, Hapo chini nimekuwekea baadhi ya nukuu muhimu zilizopo kwenye taarifa hiyo ya Kamati.
"Kamati iliyoundwa na Waziri Nape kuchunguza sakata la kuvamiwa Clouds imesema kuwa RC Makonda alichagua kwa hiari kutokufanya mahojiano nao, tulienda ofisini kwake, kamati ilipopanda ngazi mkuu wa mkoa alitokea mlango mwingine na kuondoka

Makonda alichagua mwenyewe kutosikilizwa na kamati kwa hiyo haitaathiri matokeo ya uchunguzi huu, Kamati imejiridhisha kuwa ni kweli RC Makonda alivamia kituo cha Clouds ambapo alikwenda kwa gari aliyokuwa akiendesha mwenyewe."- Balile
"Chanzo cha uvamizi ni RC Makonda kutaka kurushwa kwa kipindi alichohojiwa mwanamke anayedaiwa kuzaa na Askofu Gwajima. Kamati imethibitisha kuwa Makonda na Askari aliokuwa nao waliingia mpaka kwenye ofisi za kurushia matangazo kinyume na sheria."- Balile
"Kamati imethibitisha Makonda na Askari waliovamia Clouds waliwatisha watangazaji kuwafunga miezi sita na kutuhumiwa kwa dawa za kulevya. Kutokana na vitisho hivyo, kipindi cha SHILAWADU kwa siku hiyo hakikufungwa kama utaratibu wa kipindi unavyotakiwa sababu ya vitisho."- Balile
"RC Paul Makonda aliwatishia watangazaji wa Clouds angewafunga miezi sita au kuwataja kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya."- Balile

'Ripoti ina vielelezo vya sauti na picha za waliokuwa wanatoa ushahidi'-Waziri Nape

Waziri Nape amesema ripoti aliyoipokea ataiwasilisha kwenye mamlaka za juu ili wao waone ni hatua gani wanaweza kuchukua kwa RC Makonda.

No comments:
Write comments