Pesa hizo zilipatikana katika dawati la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanja wa ndege kuabiri ndege.
Fedha hizo, za thamani ya jumla ya dola 150,000 za Marekani, ziligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege.
Msemaji wa tume ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria Wilson Uwujaren amesema magunia hayo yalikuwa na mabunda 200 ya noti mpya, ambayo yalikuwa bado hayajafunguliwa kutoka kiwandani.
Amesema uchunguzi unaendelea kubaini nani mwenye magunia hayo
No comments:
Write comments