Rais Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi wa NASA Raila Odinga baada ya kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema hata kama amejitoa Katiba ya Kenya haizuia uchaguzi kutofanyika
Kenyatta amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo limeigharimu nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi kurudiwa anajiengua tena.
"Rafiki yangu nasikia sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka peleka zaidi ya shilingi bilioni 12 hivi sasa zinatumika ili tufanye uchaguzi, pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingetumika kujenga hospitali ya wananchi sasa zinatumika kwa uchaguzi ambao yeye ndiye aliitisha na sasa anasema hataki, kuna haki hapa jamanii, si mahakama ilisema IEBC haina makosa hayo masharti yote unatoa lakini tume hii si ndiyo imefanya viongozi hawa wengine wote kupatikana" alihoji Kenyatta
Mbali na hilo Kenyatta amesema kuwa wao wataendelea na mchakato wa uchaguzi kama kawaida na kusema huenda awepo au asiwepo Odinga uchaguzi utafanyika kama kawaida kama ambavyo tume ya uchaguzi ilitangaza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments