Makada
15 wa Chadema waliojitambulisha kuwa viongozi wa chama hicho Wilaya ya
Ilemela Mkoa wa Mwanza wamehama chana hicho na kujiunga na Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Makada hao
wakiongozwa na Damas Kimenyi aliyejitambulisha kuwa Katibu Chadema wa
Wilaya hiyo walitaja kuridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli na
mbunge wa jimbo la Ilemela, Angelina Mabula kuwa miongoni mwa sababu za
kujiunga na CCM.
Wanachama hao wapya
walipokelewa katika ofisi za CCM Wilaya ya Ilemela leo (Alhamisi) jioni
wakati wa hafla iliyoongozwa na Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Nelson Mesha.
Hata
hivyo, Katibu Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Meshack Micus amesema
waliohamia CCM walishavuliwa uongozi tangu Januari 18, mwaka huu wakati
wa kikao cha Mkutano Mkuu wa wilaya ambacho pia kilihudhuriwa na
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.
“Hao
ni wanachama wa kawaida na pengine wameondoka kwa hasira ya kuvuliwa
madaraka baada ya Mkutano Mkuu kuunda kamati ya muda ya uongozi chini ya
uenyekiti wa Warioba Wanzagi na Katibu wake Peter Kaiza,” amesema
Micus.
Wengine waliojiunga na CCM ni
Lukas Syrilo (Katibu wa Baraza la Vijana Bavicha), Agnes Majora (Katibu
wa Baraza la Wanawake, Bawacha), Lucy Kazungu (Mwenyekiti Bawacha), na
Edwine Sarung aliyejitambulisha kuwa Mweka Hazina.
Pia
wamo Philipo Richard Mjumbe wa kamati tendaji wa Wilaya, Ester Ayoub
Makamu Mwenyekiti wa wazee Wilaya, John Haule Mwenyekiti Bavicha,
Vestina Johnson Mjumbe wa Bawacha Wilaya na Yohana Emanuel Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa wilaya
No comments:
Write comments