Baada
ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha
Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema ambaye amesota gerezani kwa zaidi
ya miezi minne, amefunguka kwa mara ya kwanza kuwashukuru wale
waliompigania huku akieleza stori ya kusisimua kuhusu mtoto wake.
Lema
amedai anaenda kumuona mwanaye ambaye alitaka kufikia uwamuzi wa kutaka
kufanya kosa ili na yeye aingie gerezani kukaa na baba yake.
“Leo
nina mambo machache sana ya kuongea, ninamshukuru sana mwenyezi Mungu,
mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa chama na wananchi wote
waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke wangu, kama ningepata
nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto wangu alifikia hatua
akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na mimi gerezani, na
akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani,” alisema Lema.
Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1
No comments:
Write comments