Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea
dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.
Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya kufa au kupona.
“Mfahamu
kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea
sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,”amesema Makonda.
Makonda
alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na
sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi
kama ambavyo zinaendelea sasa.
“Huwezi
kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu
kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.
Amesema
katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la
Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu
makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio
picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.
Amesema
kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na
dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.
Amelipongeza
Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya
zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa
hizo zimepungua.
“Nitoe
pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es
Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.
Aliwaasa
wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli ambaye anafanya jitihada
kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu Kigamboni alisema
anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao haujaharibiwa na
matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana walioharibika
kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na vijana
wachapakazi.
“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na uhalifu,”amesema Makonda.
Amewataka
wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim
Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya
Kigamboni tulivu na salama.
Amewaasa
wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha
hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia vijana kuchungana
wao wenyewe.
Mkuu
wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la tamasha hilo ni
kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha vijana
kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya
mazoezi.
Tamasha
hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya
Ilala, Edward Mpogolo
No comments:
Write comments