Waziri Mkuu wa Ethiopia HAILEMARIAMU DESALEGN amewasili leo nchini na
kupokelewa na mwenyeji wake rais John Pombe Magufuli, wakiwa Ikulu
jijini dar es salaam pamoja na mazungumzo ya faragha, pia wamesaini
mikataba 15 ambayo inalenga kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
Miongoni mwa mikataba iliyosainiwa na Waziri Mkuu huyo wa Ethiopia ni
pamoja na ule wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ethiopia
wenye lengo la kupambana na wahamiaji haramu,Ushirikiano kwenye sekta ya
usafiri wa anga, utalii, viwanda hasa vya ngozi na nyama, umeme pamoja
na masuala ya kilimo.
Wakizungumza mara baada ya utiaji saini mikataba hiyo iliyosainiwa na mawaziri wenye dhamana kutoka nchi zote mbili,
Rais John Magufuli na waziri mkuu wa Ethiopia wamesema ushirikiano kati
ya nchi hizo mbili inalenga kunufaisha nchi zote mbili kiuchumi, ambapo
pia Ethiopia imekubali kufungua ubalozi wke hapa nchini.
Mambo mengine yaliyoongelewa kwenye mkutano wao wa ndani ni pamoja na
matumizi ya maji ya mto Nile, na hapa rais Magufuli anafafanua.
Rais Magufuli amempongeza waziri mkuu wa Ethiopia kwa kuonyesha nia ya
dhati ya kukuza kiswahili kwenye nchi yake ambapo wataanza kufundisha
kwenye baadhi ya vyuo vikuu.
Waziri mkuu wa Ethiopia yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo kabla
ya kuanza safari ya kurudi nchini mwake, atatembelea bandari ya Dar es
salaam ili kujionea namna wanavyoweza kuitumia bandari hiyo kusafirishia
mizigo, kwa ushirikiano na shirika la ndege la Ethiopia.
No comments:
Write comments