Saturday 25 March 2017

Msukuma : Sioni tatizo kwa Nape kuoneshwa bastola



Akihojiwa jana, Msukuma alidai kwa walichokifanya watu wanaodaiwa ni askari kumuonyesha bastola Nape ni sahihi kwani kitambulisho cha askari yeyote ni bastola au bunduki hivyo Nape hakupaswa kuwa na shaka maana walikuwa wanamlinda. Msukuma alikwenda mbali zaidi na kusema hata yeye alionyeshwa SMG nane lakini hakuwa na shaka maana wale ni askari.

Aidha Msukuma alisema kuwa Nape alipaswa kutulia kwanza hata kwa miezi mitatau ndipo angezungumza aliyotaka kuzungumza.

Pia amemsihi Nape kuacha hasira mara baada ya kutenguliwa kuwa waziri kwani wakati anaomba kura katika jimbo lake la Mtama  hakuomba na uwaziri, hivyo asilie kuenguliwa katika wadhifa huo kwani bunge lina wabunge 360 na kila mbunge angependa kuwa waziri, hivyo kuenguliwa kwake katika nafasi hiyo inawapa nafasi wabunge wengine nao kuwa mawaziri siku moja na hata yeye anatamani kuwa waziri.


No comments:
Write comments