Thursday, 16 March 2017

MTEI AFUNGUKA AWATAKA VIONGOZI KUHUDUMIA WANANCHI 2020 SI MBALI

Ndugu Mwandishi dhana ya udhaifu ni pana sana mwenyekiti kuongoza yeye miaka mingi sio udhaifu wa chama ni aina uongozi tu ila ni vyema kuwa na mabadiliko. Kupata uongozi mpya ni jambo zuri ila Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) sio dhaifu kwa kutofanya mabadiliko ya kiuongozi, ila wanachama kadhaa ndio dhaifu na nasema wamekuwa dhaifu, chama kiko imara.
Tumekuwa na ajenda nyingi ila hii unayosema wewe sio ajenda ya chama ni mambo ya mtandao tu, vyeti vina mantiki gani kwa walala hoi huko vijijini?
Wanahitaji zaidi waone umasikini umewatoka, wanahitaji sera zitakazowatia moyo na kuwa na imani na chama chetu na ninawasihi sana viongozi wangu wa chama waliopewa dhamana huko majimboni wajikite zaidi kuwahudumia wananchi 2020 si mbali sana.
Suala la vyeti sio ajenda yetu ya chama hili jambo nalisikia tu na mimi inawezekana tukawa tunacheza ngoma ya chama tawala bila kujua, tatizo vijana wanakimbilia vitu bila kujuwa undani wake, misingi ya Chadema sio kudandia matukio na kuyafanya ajenda; haya mambo yanapoteza muda unajikuta mshindani wako amekuacha mbali.
Kudandiadandia matukio ambayo hujui yanalenga nini ni aina ya kupoteza mwelekeo. Napenda wabadilike wajikite zaidi kuwahudumia wananchi, suala la vyeti inawezekana ni ngoma inayopigwa CCM halafu baadhi ya vijana wetu wanaicheza bila kujua muda unaenda bila kujuwa wanaacha mambo ya msingi.
Nawaambia viongozi turudi katika misingi ya chama, nimemshauri hata Jonathan atulie sio kila siku uko gerezani tuwahudumie wapiga kura wetu.
Mzee Edwin Mtei,
Radio Dw,
Sauti ya Ujerumani

No comments:
Write comments