Ikiwa
sasa ni takriban miaka miwili tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania
One Theatre (TOT), Kampteni John Komba, kufariki Dunia, Mtoto wake
Gerald John Komba, ameibuka na kutoa wimbo wa kuiunga mkono Serikali
katika mapambano yake mapya dhidi ya dawa za kulenya nchini Tanzania.
Gerald
aliyezaliwa mwaka 1986 jijini Dar es salaam, amesema, ameamua kutoa
wimbo huo wenye maudhi ya kwaya, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo
cha Baba yake, Marehemu John Komba aliyefariki Dunia, Februari 28, 2015
katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar e Salaam, alikopelekwa
baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake, Tangibovu kwa Komba.
Mtoto
huyo wa Jihn Komba aliyekuwa mwanamuziki nguri wa utunzi na uimbaji wa
nyimbo za kwaya, amesema, wimbo aliotoa nimarejeo ya wimbo ambao
ulitungwa na nguri huyo, kukemea usambazaji na matumizi ya dawa za
kulevya miaka zaidi ya kumi iliyopita, lakini baada ya kuurekodi
haukuwahi kuimbwa na TOT wala kuchezwa kwenye vituo vya Radio au
Televisheni.
Gerald ambaye amesomea
Sheria katika Chuo Kikuu cha Saint Augustine kilichopo Mwanza, Tanzania,
baada ya masomo ya shule ya Msingi katika shule ya Kawe “A” na shule
yasekondari Mbezi Beach High school, anasema katika kuutoa wimbo huo,
hakubabaisha kwa kuwa na yeye anacho kipaji cha kuimba japo amekuwa
hakitumii sana. Zamani Shule ya Kawe A’ ilifahamika kwa jina la
Tanganyika Packers, lakini baada ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili, Ali
Hassan Mwinyi kubaini kuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika
Packers kimeshakufa, akaamua shule hiyo kubadilishwa jina.
“Nimeanza
kupenda sanaa ya muziki tangu nilipokuwa mtoto, kwa kuwa nilikuwa
naenda na Baba (John Komba) kwenye maonesho yake na kundi la TOT, na
nilikuwa navutiwa sana na namna baba yangu alivyokuwa akitamba jukwaani
wakati akiimba”, alisema Gerald.
“Tangu
wakati huo, nilikuwa napenda kukariri nyimbo zote za Baba, na hakuna
wimbo nisioujua kuanzia ala hadi mpangilio wa mashairi, lakini pia pia
shuleni nilikuwa naimba kwenye kwaya ya shule, na siku za karibuni
nimekuwa pia nikiimba kwaya kwenye Kanisa la Praise team, hapa jijini
Dar es Salaam”, aliongeza.
Anasema,
ameambua kuurudia wimbo wa Marehemu Baba yake kwa sababu, kwanza yeye
binafsi anachukia mamia ya vijana wanavyoharibika kwa matumizi ya dawa
za kulevya kwa namna ambavyo wanatumiaji wengi wa dawa hizo hukatishwa
ndoto zao mbalimbali za kuwa watu muhimu katika ujenzi wa taifa la
Tanzania.
“Kwanza ukizingatia hakuna
aliyezaliwa teja, wengi wanaokuwa hivyo wanakutana na hili balaa
wanapoingia kwenye jamii kwa hiyo nikaona nifanye kitu ili jamii iweze
kutoa mchangu wangu katika kuelimisha jamisha jamii ili izinduke na
kuelewa namna dawa hizi za kulevya zilivyo za hatari.
Pili
niliamua kuurudia wimbo huu kwa sababu, watu wengine hasa Walimu na
Wazazi wengi wao wanajisahau katika kusimamia malezi ya vijana. Wazazi
wanamwachia Mwalimu jukumu la kutazama mwanafunzi akiwa shule bila kujua
mtoto anaharibika katikati ya shule na nyumbani wakati wa kwenda na
kurudi nyumbani, kwa hiyo Mwalimu na mzazi ni Watu muhimu wa kuchunga
mwanafunzi”, alisema Gerald.
Anasema,
sababu yake ya tatu ya kuamua kuurudia na kuongeza vionjo kwenye wimbo
huo ni kusisitiza kuwa mapambano hayo ni ya Watanzania wote ambapo
anasema ameweka baadhi ya majina ya wakuu wa mikoa kwenye wimbo huo kwa
kuwa vita hii ya mapambano dhi ya dawa za kulevya ni ya Watanzania wote
na hao ndiyo wawakilishi wa Rais kwenye kila mkoa.
“Nimeongeza
vionjo kwa kutaja hawa wakuu wa mikoa kwa kuwa najua hawa ndiyo
waakilishi wa Rais, na Rais Dk. John Magufuli hawezi kukabiliana nayo
peke yake hivyo unahitajika ushirikiano na wananchi kuanzia ngazi ya
Kaya, Vijiji, Kata, wilaya hadi mkoa.
Na
mwisho niliamua kuurudia kama Kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha
Marehemu Baba, ukiuusikiliza wimbo huu utangua kuwa sauti yangu na yake
zimefanana kwa karibu sana katika uimbaji, hivyo itaweza kuashiria kuwa
yale alyolenga kuyakemea kwenye nyimbo zake, hata baada ya kufariki
dunia lakini bado kuna mtu mwingine ambaye ni mtoto wake atakayeendelea
nyimbo hizo kufanya lengo lake la kuionya jamii ibaki pale pale”,
alisema Gerald
“Mtindo nilioutumia
kwenye wimbo huu ni uleule wa kwaya aliotumia Baba, na nimeuimba upya
kwa kushirikiana na Mama yangu Mzazi, Jane Mkondwa ambaye ni mwimbaji wa
miaka mingi katika Kundi la TOT, Nimeurekodi katika Studio za PM
Records chini ya Mtayarishaji anayefahamika kwa jina la Testimony.
“Baadhi
ya maneno yaliyomo kwenye wimbo huu ni maneno ambayo ambayo hutumiwa
zaidi na mateja na nimefanya hivyo kwa kuwa ni miongoni mwa walegwa
katika vita hii. Hivyo, nikaona nitumie maneno wanayoweza kuyaelewa
haraka kama; ‘nywele misumari’, ‘twende kilioni’, ‘Macho kufutuka’,
‘akili inayeya’ ambapo neno kama akili inayeya kwa teja humaanisha
anavyokuwa baada ya kulewa dawa za kulevya yaani ufahamu katika akili
zake unapotea.
“Maneno mengine ni
Gheto na Washkaji (nyumba wanapoishi vijana wa kiume au wa kike, lakini
neno mshkaji au washkaji unategemea na umri, wale wa miaka ya 1960
walimaanisha wanawake wao lakini wa sasa wanamaanisha marafiki wao
ingawa maana zote mbili zina maana sawa”, anafafanua Gerald.
Anasema,
kwa sasa wimbo huo bado upo katika sauti tu (Audi), kwa kuwa hajapata
uwezo wa kuurekodi katika video, ingawa yupo katika jitihada za kutafuta
uwezo ili kuhakikisha anaurekodi katika video ili ujumbe uweze kufika
kwa urahisikwa walengwa wote.
Gerald
anatoa mwito kwa Watanzania kuungana ili tulitokomeza usambazaji na
matumizi ya dawa za kulevya bila kujali itikadi za vyama, kabila, jinsia
kwa kuwa ni janga linaloweza kuingia katika familia, Taasisi, Chama cha
siasa, kabila au jinsia yoyote.
“Watanzania
wenzangu naomba kila atakayepata fursa ausikilize kwa makini wimbo
wangu huu, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli
katika mapambano haya mapaya dhidi ya usambazaji na matumizi ya dawa za
kulevya katika nchi yetu ya Tanzania”, anasema Geral
No comments:
Write comments