Juhudi za kuutafuta mwili wa raia wa Uingereza anayemiliki shamba kubwa
ambaye alipigwa risasi na wafugaji waliojihami nchini Kenya wikendi
iliopita mjini Laikipia zimefeli baada ya watu waliokuwa wamejihami
kulifyatulia risasi kundi la wasakaji waliotumwa na familia yake
kulingana na gazeti la the Star nchini Kenya.
Tristan Voorspuy aliuawa na wafugaji wakati alipoenda kuchunguza baadhi
ya nyumba zake ambazo zilikuwa zimechomwa na washambuliaji hao.
Laikipia na kaunti jirani zimekuwa zikikabiliwa na viwango vya juu vya
ghasia zinazosababishwa na wafugaji ambao wanatafuta lishe ya mifugo yao
lakini, wachanganuzi wanasema kuwa utovu huo wa usalama umesababishwa
na siasa.
Wamiliki wa mashamba makubwa mjini Laikipia wameitaka serikali kueka usalama katika eneo hilo.
Wanahofia kwamba tatizo hilo huenda likaenea katika kipindi cha wiki
zijazo huku ardhi ya lishe ikipungua katika maeneo ya wafugaji hao
kutokana na ukame katika maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo.
No comments:
Write comments