Baraza
la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi
kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa
kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.
Tangazo
hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua
ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti
ambavyo sio vyao.
Kwa mujibu wa
tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu
watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao
kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.
Wananchi
wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa
saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu
hadi Ijumaa.
Aidha, tangazo hilo
limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia
barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za
kazi.
Tangazo hilo linaendelea kutoa
msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016
la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa
mzigo kwa Serikali yake.
No comments:
Write comments