Kingunge ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na MTANZANIA
Jumapili, amewataja viongozi hao wa juu wanaopaswa kuadhibiwa kwa
usaliti kuwa ni Mwenyekiti Mstaafu, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti
Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.
Aidha, kuhusu kilichotokea ndani ya CCM, kufukuzwa kwa baadhi ya
Makada wa Chama hicho kwa tuhuma za usaliti, Kingunge amesema kuwa kitu
hicho si kigeni kwani ni mwendelezo wa makosa yaliyojitokeza kwenye
mchakato wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2015.
“Sophia Simba alimsaliti nani? Madabida kamsaliti nani? na katika
ngazi gani? ndiyo maana nasema hili lote ni mwendelezo wa yaliyotokea
2015 kule Dodoma,”amesema Kingunge.
Hata hivyo, Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa nchini amesema kuwa
anastaajabu sana kuona baadhi ya wanachama wanafukuzwa na wengine kupewa
onyo kali kwa kile kinachoitwa usaliti, kwani wahusika wakubwa wa
usaliti bado wamo ndani ya chama hicho na hawajaguswa na adhabu
Sunday, 19 March 2017
MZIMU WA CCM WAZIDI KUMTESA KINGUNGE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments