Jukwaa la katiba ambalo kazi yake kubwa kuratibu maswala
ya katiba, leo limetoa msimamo wao kwa mwenendo wa katiba
iliyosimama kwa lengo la kuhamasisha iweze kusimaiwa iili ipatikane
katiba mpya.
Jukwa hilo lili ratibu mkutano mkubwa watu zaidi ya 150
waliweza kuhudhuria wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wabunge,
viongozi wa dini pamoja na asasi za kiraia. Lengo liliwa kuwakumbusha
juu ya katiba ambayo imesimama. Maadhimio ambayo Jukwaa imeyaona pamoja
na kuomba kukutana na Rais John Pombe Magufuli lengo likiwa kumueleza
namna katiba ilivyomuhimu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Kwa nafasi aliyo nayo John Pombe Magufuli kikatiba yeye
ndiye mtu pekee kwa sasa mwenye uwezo wa kuamua hatma ya kuokoa ama
kuangamiza mchakato wa katiba. Licha ya kuomba kukutana na mkuu wa nchi
pia jukwaa limeazimia vyombo wa habari kupata fursa ya kutangaza
kuwezesha kuendelea kutoa elimu juu ya hsitoria ya mchakato wa katiba
pamoja na muadhui ya katiba.
Pia imeomba waziri wa katiba nasheria Dkt Harrson
Mwakyembe aandae na kupeleka miswada ya marekebisho katika sheria mbili
zinazo ongoza mchakato wa katiba mpya
No comments:
Write comments