Friday 31 March 2017

Rais Zuma awatimua mawaziri 15 waliotaka kumpindua


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi baadhi ya mawaziri nchini humo.
Waziri wa fedha Pravin Gordhan na naibu wake Jonas Mkabasi wamefukuzwa kazi pia.
Chanzo cha mabadiliko hayo baada ya kuwa na fununu kuwa huenda bwana Gordhan alikuwa na mpango wa kuipindua serikali.
Kwa mujibu wa habari Malusi Gigaba ndiye ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.
Mawaziri takriban kumi na tano wamefukuzwa kazi na rais Zuma,jambo ambalo sio la kawaida.
Hata hivyo kumekuwa na vipingamizi kutoka chama tawala kuhusu ufutwaji kazi wa Pravin Gordhan.

No comments:
Write comments