Roma amekanusha madai ya mashabiki wa muziki kuwa ameufyata mkia na
kuacha kuichana serikali kwenye nyimbo zake kama zamani kutokana na
serikali ya awamu ya tano kuto’entertain’ mambo hayo!
Rapper huyo amedai kuwa muziki anaofanya sasa hautabiriki na ataendelea
kuwashtukiza mashabiki kwa nyimbo wasizotarajia kutoka kwake.
Kwenye mahojiano na kipindi cha Extra Fleva cha Uplands Fm, Roma amedai
kuwa si mara ya kwanza mashabiki kusema ameufyata. “2012 ile ndio
ilikuwa noma, kwasababu ndio nakumbuka ndio nilikuwa nimeachia
Mathematics halafu tukachukua tuzo mbili halafu nikakaa kimya mwaka na
miezi nane,” amesema.
“Ndani ya kipindi hicho zilitokea sana kuliko hata zinazotokea sasa hivi
‘yaani huyu Roma ndio hawezi kufanya chochote, ameshapewa hela, Roma
ametishiwa, Roma amepelekwa polisi, Roma amepelekwa ikulu’ yaani
ziliongelewa sana halafu siku isiyokuwa na jina wakasikia 2030 watu
wakasahau yote waliyoyasema,” ameongeza.
“Baada ya mwaka mambo yote yakapita wakasahau, wakarudia tena kuongea, siku isiyokuwa na jina wakaja wakasikia Viva Roma.”
Kazi za hivi karibuni za Roma zimeonekana kuwa na mrengo tofauti
ukilinganisha na zile alizokuwa akizitoa miaka ya nyuma. Kwa sasa nyimbo
zake zinazofanya vizuri ni Usimsahau Mchizi akiwa na Moni Central Zone
na K aliyoshirikiana na Baghdad.
No comments:
Write comments